Presented by: Felix Luboya
Website : www.newadvent.org/fathers/0108.htm
BARUA KWA WAFILADELFIA
1 SALAMU
Ignasius ambaye pia anayeitwa Teoforus, kwa kanisa la Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu kristu huku filadelfia, ambalo limepta huruma na kusimikwa katika amani na kufurahi bila kuchoka mateso ya Bwana, na ambalo limejawa na huruma ya roho mtakatifu kwa njia ya ufufufko wake, ninawasalimu katika damu ya yesu kristu ambaye ni wa milele na furaha isiyo na kifani ,hasa watu wanapokuwa na muunganiko pamoja na askofu, makasisi na mashemasi, ambao wamechaguliwa kulingana na matakwa ya Yesu Kristu ambaye ameimarisha ulinzi katika Roho Mtakatifu.
2 SIFA YA ASKOFU
Kwa ufahanu wangu ,Askofu amepata utume ambao umefunganika katika kitumikia mafao ambayo si kwa ajili yake au baadhi ya watu bali kwa ajili Gal 1:1 ya upendo wa Baba, na Yesu Kristu ambapo ninashangazwa na huruma yake, na kwa hakika kwa njia ya ukimwa wake ameweza kukaminlisha mpango wa ukombozi kwa kuwazidi hasa wale waongeaji sana. Kwa sababu hiyo moyo wangu watangaza mapenzi kwa Mungu aliye furaha na ufahamu wa fadhila na ukamlifu na ambapo kudumu kwa huruma yake huonekana.
3 KUDUMISHA MUUNGANIKO NA ASKOFU
Kwa hakika ninyi ni watoto wa mwanga na ukweli, msiukubali mgawanyiko miongoni mwenu na mafundisho potofu, ila mnapaswa kutambua kuwa palipo na mchungaji kuna kondoo, muwe macho maana kuna mbwa mwitu watatokea kuwa wema, watabeba mateka 2Timoteo 3,6 wale watakao mkimbilia Mungu, lakini katka umoja wenu hawatapa nafasi
4 EPUKENI KUJITENGA.
Mjiweke mbali na yale yalyo mabaya ambayo Yesu kristu hakufundisha, kwa sababu sio yale yaliyopandwa na Baba. Si kwamba nimekuta mmegawanyika ila mna usafi sana. Mara nyingi walio na Mungu na Kristu wako siku zote na Askofu. Na mara nyingi kama itakavyokuwa katika kufanya toba watarudi katika umoja na Kanisa nao pia watakuwa wana wa Mungu katika kuuishi ukweli wa Kristu yesu. Msitende dhambi wapendwa. Kwa yeyote yule atakayemfuata aliyejitenga na kanisa kwa hakika hawezi kuuridthi ufalme wa Mungu. Kwa yule atakaetembea katika mafundisho mageni kwa hakika hakubaliani na mateso ya Yesu Kristu
5. EKARISTI NI MOJA TU.
Mnapaswa kuwa na Ekaristi Moja. Kwa sababu kuna Mwli Mmoja wa Bwana wetu Yesu Kristu na Kikombe Kimoja kinachoonesha umoja wa Damu yake na altale , kama ilivyo Askofu mmoja, makasisi na mashemasi watumishi wapendwa. Kwa hiyo yote myafanyao muyafanye kadiri ya matakwa ya Mungu
6. MNIOMBEE.
Wapenzi, ninazidi kuwapenda na kufurahi kwa ajili yenu. Ninatafuta kuulinda usalama wenu, ila ninaogopa kwa sababu ya mapungufu yangu ambayo hayaafikiani na Yesu ambaye ni mkamilifu. Ila sala zenu kwa Mungu zitanifanya niwe mkamilifu ili niweze kuipata ile sehemu ambayo kwa huruma yake nimetayarishiwa, kama ninavyoikimbilia injili ambayo ni Mwili wa Yesu kama kwa mitume na makasisi wa kanisa. Pia tunapawa kuwapenda manabii amabao wameitangaza injili na kuweka matumaini katika Yeye na wakamsubiri,(Yohane Mbatizaji) ambapo nasi tunaamini waliokolewa kwa kuwa na umoja naye katika utakatifu wa maisha yao, na yenye upendo na mastajabu , na baada ya kuwa na ushuhuda wa kuzaliwa kwa Kristu Yesu na kutambuliwa nasi katika kuitangaza injil.i
7 MSIKUBALI UYAHUDI
Kama mtu yeyote akiwahubiria sheria ya kiyahudi, ni heri msimsikilize. Ni vema kusikliza mafundusho ya kikristo toka kwa aliye tahiriwa kuliko yule wa kiyahudi ambae hajatahiriwa. Mzikimbie njia mbaya na mitego ya wafalme wa dunia. Mjitahidi kujiweka katika moyo ule usiogawanyika. Na ninamshukuru Mungu kwa kuwa na dhamiri iliyo stahilifu, na hakuna kati yenu anayesjisifia kwa kuwa alivyo, ila inawezekana katka Mungu
8 NINAWAHIZA KATIKA UMOJA
Kama ilivyo kwa wengine wengependa kunidanganya kwa sababu ya ubinadumu wangu, lakini haiwezekani hata siku moja kumdanganya Roho Mtakatiu, kwa sababu Yeyé anajua na kutujua, pia anatambua siri zetu ndani ya roho zetu Jn 3:8. Pindi nilipokuwa miongoni mwenu nililia na kuongea nanyi kwa sauti ya ukali. Tafadhali sana, msikilizeni Askofu, Kasisi na Mashemasi. Watu walipatwa na wasiwasi juu ya yale niliyoyasema kuhusu mgawanyiko miongoni mwenu. Kwa kweli huu ushuhuda si shauri ya uwezo wangu wa kiakili bali ni ufunuo toka kwa Roho Mtakatifu. Kuwa msifanyechochote bila Askofu.Itunzeni miili yenu kama hekalu la Mungu; pendeni umoja, epukeni mgawanyiko; muwe wafuasi kweli wa kristu kama alivyo kristu na Baba yake.
9.UJUMBE UNAENDELEA
Kwa hakika nilijitahidi kufanya kile kilichoniangukia kama mtu wa ibada na sala kwa ajili ya umoja. Kwa hakika palipo mgawanyiko na hasira Mungu pia hayupo. Kwa wale wote wanaofanya toba ya kweli na kujirudi katika muungano na Mungu na Askofu, Bwana huwasamehe. Ninawakabidhi katika neema ya Bwana Yesu Kristu ambayo itawaweka huru.Ninawashauri msifanye maamuzi katika hali ya hasira ila kulingana na mafundisho ya Kristo. Niliwasikia baadhi yenu wakisema kuwa hawataamini mafundisho ya Kristo, kama wasipoyakuta katika maandiko ya mafundisho ya kale, niliwajibu na kuwaambia kuwa yameandikwa. Kwangu Yesu ni ukamilifu wa mafundisho yote ya kale: Msalaba,Kifo na Ufufuko wake na imani katika yeyé haya yote yanaratibiisha uzuri wa kale
10 AGANO LA KALE NI ZURI :AGANO JIPYA NI ZURI ZAIDI
Makuhani ni wazuri, ila Kuhani mkuu ni mzuri zaidi, ambaye kwaye mtakatifu wa watakatifu anahusishwa na ambaye kwaye tu, amekabidhiwa siri zote za mbinguni. Yeye ni mlango wa Baba ambamo tunapita kuelekea kwa Abrahamu, Isaka, Yakobo,Manabii,Mitume na Kanisa. Wote hawa wanatuwezesha kuupata ule muunganiko na Mungu. Ila injili inamiliki kitu ambacho fikra zetu zinashindwa kukielewa:Uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristu, mateso na ufufuko wake.Wapendwa wetu manabii walimtangaza, ila Injili ni ukamilifu usiokufa. Vitu vyote ni vizuri kama ukiamini katika upendo
11 PONGEZI KWA WAANTIOKIA KWA KUDUMU KATIKA UMOJA NA HASA WAKATI WOTE WA MATESO NA MACHAFUKO
Kwa sala zenu na huruma ya kristu Yesu. Nimepata tarifa kuwa Kanisa la Antiokia lililoko Siria lina amani tele; huu kwa sasa ,utakuwa wajibu wenu kama Kanisa la Mungu kumchagua shemasi, kama balozi wa Mungu kwa ajili yenu na wengine, ili afurahi nanyi pindi mnapokuwwa pamoja katika kulisifu na kulitukuza jina la Mungu. Mbalikiwa, ni yule anayemtumikia Kristu Yesu na kumtukuza na Mungu. Na mnapaswa kufahamu kuwa mnachokifanya si kwa utukufu wenu bali kwa utukufu wa Mungu Baba.
12 SHUKURANI NA SALAMU
Kama ilivyo kwa shemasi Filo wa Silisia, mtu mwenye ibada na heshima ambaye alikuwa mtumishi kwangu wa Neno la Mungu, pamoja na Rheus Agothapus ambaye aliyenifuata toka Siria, bila ya kujali thamani ya maisha yake, huu ni ushuhuda kwa niaba yenu, nami ninampatia Mungu Shukurani kwa ajili yenu kuwa mliwapokea. Kwa neema na huruma ya Yesu Kristu wasamehewe wale wote wanaowadharau ninyi. Wapendawa ndugu zenu wa Troas wanawasalimia; Nami kwa heshima yake na upande wangu ninawaandikia ujumbe kupitia Burrhus aliyeletwa kwangu na Waefeso na Wasirmia. Kwa heshima na utukufu wa Kristu ambao unaonekana kwao na ambao kwaye wanamtumaini katika mwili, roho, imani na upendo. Nami ninawatakia kila la heri katika Kristu na tuendelee kuwa na Tumaini lile lile la Msingi.